....

....

WATU WENYE UWEZO MKUBWA "SUPER HUMAN" WALIOWAHI KUTOKEA

No Comments
 Uwepo wa watu wa ajabu  mara nyingi tumeuona kwenye filamu (movies). Lakini hawa wafuatao ni baadi ya watu ambao wana uwezo wa ajabu.

1. Natasha Demkina ni msichana kutoka Urusi. Huyu anadai kuwa na uwezo wa kuona kama X-ray. Yeye ana uwezo wa kuona ndani mwili wa mtu na kuona kama una tatizo au lah! Uwezo wake huo uliweza kujitokeza alipokua na miaka kumi.
Demkina anasema "Nilikuwa nyumbani na mama yangu ghafla nikaanza kuona tofauti. Niliweza kuona ndani ya mwili wa mama na nikaanza kumweleza viungo nivionavyo, Sasa ninaweza kubadili kutoka kuona kawaida na kuona kinamna nyingine(ambayo Demkina anaita medical vision). Kwa mda wa sekunde naweza kuona vitu vya rangi ndani ya mwili wa binadamu kisha naanza kuvichambua".

2. Jina lake ni Saadiya Saleh miaka 12. Ni msichana mmoja kutoka Yemen aliyewashangaza madaktari, msichana huyo analia matone ya mawe badala ya machozi. 
Wanakijiji wenzake wanasema kuwa anatumiwa na mashetani. Ila daktari alishindwa kutoa maelezo ya kujitosheleza kwani alisema Saadiy anaumwa ugonjwa ambao bado hautambuliki.

3. Ben Underwood
Huyu kijana yeye ni kipofu ambaye hutumia mwangwi katika kufanya mambo yake na wanamwita "Super Echolocation ".Ben alipatwa na ugonjwa wa macho alipokuwa na miaka miwili, ugonjwa ambao alipofika miaka 3 ulimsababishia kuondolewa macho.
Ben alipokuwa na miaka 5 alianza kuweza kugundua uwepo  wa vitu vinavyomzunguka kwa kutoa kelele za mwaliko wa sauti (clicking noises) kwa ulimi.
Ben Underwood
Na amefikia hatua ya kuweza kucheza mpira wa kikapu, kutembea na vibao vyenye matairi ' Rollerblading', mpira wa miguu, hata kucheza michezo ya video.

4 .Michel Lotito

Michael Lotito amezaliwa juni 15, 1950 na kufariki June 25, 2007. Amezaaliwa huko  Grenoble, Ufaransa pia anajulikana kama bwana mla vyote ( Mr. Eat All). Ana uwezo wa kula chuma, glasi,mpira na vitu vingine.
Akiwa nakula vitu hivyo kwa kuvivunja kwanza vipande vidogo vidogo na kula kisha kunywa na maji
  Loito alijijua kua yeye ana uwezo wa ajabu kipindi alipokuwa na umri wa miaka 9 siku aliyopokea simu kisha akaanza kutafuna seti ya television.
Unene tumbo la Michel Lotito ni mara mbili ya binadamu wa kawaida.

back to top