....

....

JINSI YA KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO

No Comments

Inaweza ikafikiriwa kuwa hakuna chchote kiancho weza kufanyika huhusu msogno  wa mawazo. Kuwa na amani katika maisha ni haki
  yako, ni vizuri pia na huchukua mda mchache sana ili uwe na amani. Na binnadamu ana uwezo mkubwa wa kuondoa msongo wa mawazo zaidi vile afikiriavyo.

1. Kwanza Tambua chanzo cha Msongo wa Mawazo
Kwa kuanza kujua chanzo cha mawazo ni kitu kizuri ila wakati mwingine inakuwa sio rahisi kama unavyofikiria. Hii inawezekana kwa kujiangalia tabia, fikra na visingizio. Jiulize
  • Msongo huu wa mawazo ni kwa mda mfupi tu?
  • Je msongo huo unaathiri vipi maisha yako au kazi?
  • Je unawaalaumu watu kutokana na msongo huo wa mawazo au unachukilia kama hali ambayo unatakiwa kupambana nayo? 
2. Fanya Tafakari ( Meditation)
Meditation ni kitendo cha kufundisha ubongo kukumbuka na kutafakari. Pia Kufanya tafakari  husaidia kuongeza uwezo wa damu kuzunguka vizuri katika ubongo. Fanya tafakari angalau dakika 30 kwa siku ila sio lazima iwe kwa mara moja inawezekana ukaigawanya kwa dakika kumi kumi mara tatu  kwa siku. Ila unashauriwa pale unapoamka ndo ufanya tafakari.
Jinsi ya kufanya ni rahisi sana. Kaa chini unyooke na miguu ukiwa umeikunja sakafuni. Fumba macho na utulie kimya ikiwezekana ongea taratibu kwamba "Najisikia amani"  au "Mimi najipenda sana". Weka mkono tumboni (pendelea kitovuni) sugua taratibu huku ukivuta pumzi ndefu na kuhema kwa mda wa kama dakika tano. Unaweza ukaona kama ni kitu cha kwaida sana lakini husaidia

3. Usiwaze chochote bali uwe katika wakati ulipo
Hii ina maana kwamba. Inua kichwa na uhisi hewa inayokugusa katika uso. Kama unatembea sikiliza jinsi unavyotembea na usilize mshndo wa miguu yako. Kama unakula furahia radha ya chakula unachokula. Kikubwa hapa ni mawazo na akili viweke katika jambo lililopo au linalokuzunguka.
Pia katika hili swala la kuwa katika wakati uliop, unaruhusiwa pia kusikiliza mziki. Mziki huleta mhemko chanya kwenye ubongo na mwili pia kusikiliza mziki hupuguza cortisol (hii ni homoni inayohusiana na kuleta msongo wa mawazo)

4. Usiwe peke yako
Kufanya tafakari unahitajika kuwa peke yako lakini kama huwezi basi usiwe peke yako. Kuwa kijamii na sehemu mojawapo ya kuondoa msongo wa mawazo  waeleze watu unaowaamini kuusu tatizo lako yawezekekana uso kwa uso au kupitia simu.

5. Jingandamue
 Hii ni kwa kujifunga kitu chenye joto shingoni (kama kitambaa) kwa mda wa dakika kama 10. Kipindi unafanya hivyo funga macho yako na utulie. Au pia unaweza ukamwambia mtu akukande (massage) au ukajifanyia  mwenyewe kwa kujikanda shingo.

6. Fanya kitu kitakacho kufanya ucheke
Kicheko huachia "endorphins". Endorphins ni mojawapo ya kemikali zinazopatikana katika ubongo zinazoitwa 'neurotransmitters' pia hupatikana katika teza za pituitary. Msongo wa mawazo na maumivu ndio vitu ambavyo hufanya kuachiwa kwa endorphins ambayo huenda kuzuia vitu vinavyotafsiri maumivu ( opiate receptors ) katika ubongo ili kupunguza ukubwa wa maumivu au mawazo. Hizi kemikali hufanya kazi sawa na madawa kama vile morphine na codeine ila endorphins haikuathiri (addicted).
Kwa hiyo fanya kitu au angalia kitu kitakachokuchekesha au kukufurahisha sababu kicheko hufanya endorphins kuachiwa kwa wingi ili kupunguza msongo wa mawazo na mauvimu.


back to top