Hawa ndio watu wenye uwezo wa kufkiri waliowahi kutoke hapa duniani.
10. Stephen Hawking
Alizaliwa mwaka 1942, Ni mwanasyansi wa nadharia na kosmolojia (Syansi Kuhusu ulimwengu). Stephen anasumbuliwa na ugonjwa ambao hushambulia misuli kataamu unaitwa 'amyotrophic lateral sclerosis (ALS)' ugonjwa ambao hivi sasa umemfanya kupooza. Uwezo wake wa kufikiria ni 160.
9. Albert Einstein
Huyu ni mwanafizikia alyeleta nadharia isemayo kwamba vipimo vya mwendo, nafasi na wakati vinawiana/kadiriana.
8. Judit Polgar
Ni mwanamke toka Hungary aliyezaliwa mwaka 1976. Yeye anasifika kwa kucheza mchezo unaoitwa sataranji (Chess).
Na mchezo huu kaujua kwa sababu alikuwa akifundishwa na baba yake tangu utotoni
7. Leonardo Da vinci
7. Leonardo Da vinci
6. Marilyn Vos Savant
Huyu ni mwandishi wa habari anayeshughulikia mada au makala maalum (Columnist), mtunzi mwenye kuandikwa mara tano katika kitabu cha "Guinness Book of World Records" kuwa ni mwanamke pekee mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri ambaye hakuweahi kutokea. Uwezo wake wa kufikiri unafikia 190.
5. Garry Kasparov
Kama ilivyo kwa mwana mama Judit Polgar, Garry pia ni mcheza sataraji (Chess) asiye fungika aliyeanza mchezo huo akiwa na miaka 11. Uwezo wake wa kufikiri unafikia 190. Garry aliweza kumfunga mcheza sataranji maarufu aitwaye Azerbaijan (Aliyeweza kuifunga supercomputer ambayo yenye uwezo fikiria kete ya kwanza kucheza mpaka ya million 200 kwa sekunde). Lakini mbele ya Garry mababe huyo aliyezunguka duniani (Karibia nchi 75) kutafuta mchezaji aliweza kufungwa.
4. Kim Ung-Yong
Huyu ni mhandisi kutoka korea aliyezaliwa 1963. Uwezo wake wa kufikiri unafikia 210. Akiwa na miezi 6 tangu azaliwe alianza kuongea. Pia aliweza kujifunza lugha nyingi (Kijapani, Kikorea, Kijerumani na Kiingereza) akiwa na umri mdogo
3. Christopher Hirata
Ni mwana-astrofizikia (sayansi ya hali ya nyota kikemikali na kimaumbile) mwenye uwezo wa 225. Akiwa na umri wa miaka 13 alikuwa ndiye mshindi pekee mdogo aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya fizikia. Alianza kufanya kazi na shirika la anga la Marekani (NASA) akiwa na umri wa miaka 16.
2. Terence Tao
Huyu alizaliwa mwaka july,1975 huko Australia. Akiwa na miaka 16 tu aliweza kupata shahada ya kwanza (bachelor's degree) na ya pili (Master's degree). Uwezo wake wa kufikiri upo kati ya 225 na 230.
Hivi sasa Terence ni anafundisha Chuo kikuu cha California, Los Angeles.
1. William James Sidis
Mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri ambaye hajawahi kutokea. uwezo wake upo kati ya 250 na 300. Alizaliwa April 1888 huko New york. Akiwa na miaka 6 alianza "grammar school" (huku kwetu shule ya sekondari) na alimaliza ndani ya miezi 7. Akiwa na miaka 9 alikuwa tayari ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Marekani, Havard. Akiwa na miaka 11 alikuwa anajua karibia lugha 40.
Alifariki mwaka 1944 kutokana na madhara katika ubongo.