....

....

WAFANYA MAUAJI HATARI WALIOWAHI KUTOKEA

No Comments
Unaweza ukafikria kuwa ni ushetani,waliochanganyikiwa au wana upungufu wa akili. Lakini inakuwaje mtu akafanya mauaji? Wakati mwingine unaweza ukahitaji jibu ambalo hulitaki. Hawa ni wauaji hatari wa mauaji mfululizo waliopata kutokea hapa duniani.
1. Dennis Nilsen
Amezaliwa mwaka 1945. Huyu ni muuaji aliyebandikwa majina kama vile Muuaji wa vilima vya Muswell na majina mengine kama vile Muuaji mwenye huruma. Denis alikuwa muuaji basha ambaye
kati ya mwaka 1978 na 1983 aliua mashoga 15 katika jiji la London huko uingereza. Baada ya mauaji aliifadhi miili hiyo kabla ya kuikatakata vipande vipande na kuichoma moto kisha kuitumbukiza chooni. Baadaye alikuja kukatwa sababu nyama nyama za watu zilikuja kuoneka katika mifereji ya maji machafu.
Mwaka 1983 ndipo alikutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha.

2. Jeffrey Dahmer
Huyu alikuwa anajulikana kama "Milwaukee Mla nyama za watu" . Huyu anatokea marekani alizaliwa mwaka 1960. Jeff alikuwa mbakaji, muujaji na mkataji viungo vya watu 17 na pamoja watoto kati ya mwaka 1978 na 1991. Pia aliehukumiwa kwa kuua na kula nyama za watu. Alikatakata viungo kisha akavipika hapo hapo nyumbani  kwake na kuvila.
Dahmaer alikamatwa akiwa katika pilika za kuua mtu mwingine ndipo alipozidiwa nguvu na mtu huyo na pia mtu huyo kutoa taarifa polisi. Mwaka 1992 alikutwa na hatia ya kufanya mauaji 15 na kufungwa kifungo cha maisha.

3. Richard Ramirez
Alizaliwa mwa 1960 huko Texas. Vyombo vya habari vilimpa jina la "Mnyajiati wa usiku". Katika kufanya mauaji alitumia silaha mbali mbali akiwemo bunduki, visu, mapanga na nyundo. Alikuwa muuaji na muabudu ushetani, alikuwa anavamia nyumba na kuua, kubaka au kuchoma watu visu.Alikamatwa mwaka 1985 na alihukumiwa kifo lakini alikutwa amekufa katika mahubusu yake kutokana na matatizo ya kansa ya damu.

4. Peter Sutcliffe
Alizaliwa  Juni 1946. Huyu pia muuaji kutoka uingereza. Huyu yeye alikuwa anawalenga wanawake wanaojiuza katika miji ya Leeds na Bradford Mwaka 1983 alikutwa na kosa la kuua wanawake 13 na kujaribu kuua wengine 7. Mwaka 1981 alikamatwa kwa kosa la kuendesha gari lenye namba ambazo si halai za usajili na alipoulizwa kuusu mauaji alikiri.
Alikatwa na alifungwa kifungo cha maisha katika jela ya hospitali ya watu wasio na akili timamu

 5. Arthur Shawcross

Alijulikana kama muuaji wa mto  Genesse. Shawcross alizaliwa mwaka 1945 Rochester Newyork. Alikutwa na mashitaka ya kumbaka na kumua mtoto wa miaka 10. Alifungwa kifungo cha miaka 12 ambapo mwakaka 1988 alitoka. Baada ya kutoka jela siku chache baadaye aliwaua kikatili wanawake 12 wanaojiuza walio kati ya umri wa miak 22 na 59. Ailpokatwa alikiri kuua watu hao kisha mahakama ikampa kifungo cha miaka mia mbili hamsini (250) jela. Lakini mwaka 2008 alifariki.








back to top